mahakama ya Murang'a yatoa uamuzi kuwa wadhifa wa naibu spika wa bunge la kaunti hautambuliki kisheria

Baada ya mahakama ya Murang'a kutoa uamuzi kuwa wadhifa wa naibu spika wa bunge la kaunti hautambuliki kisheria mswada umewasiliswa bungeni kuweka wazi majukumu ya bunge la kaunti, ofisi ya Naibu Gavana na naibu spika ambayo kwa muda imetajwa kukosa maana na kuwatia tumbo joto wanaoshikilia nyadhifa hizo. Aidha mswaada huo utalenga kufafanua mbinu ya kuwaondoa wanachama wa bunge la kaunti, kuwekwa wazi mbinu na sababu anazotumia Gavana kumfuta au kuwaajiri wafanyakazi na maafisa wa kaunti, vilevile mfumo wa kuwaajiri maafisa hao. kikao hicho na kututayarishia taarifa hii.

Mswada huo umewasilishwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Aden Duale baada ya kupitishwa na bunge la seneti.

Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa amesema uamuzi huo wa mahakama umesaidia pakubwa kwani iwapo mswaada hupo utapitishwa sasa manaibu Spika watakuwa na majukumu.

Vilevile Duale amesema ukipitishwa, mswada huo utahakikisha maafisa wa kaunti hawaachishwi kazi na gavana mpya anapoingia ofisini na uajiri unafanywa kwa misingi ya tajriba wala si uhusiano na magavana au viongozi wakuu wa kaunti.

Wakizungumzia uchaguzi wa manaibu gavana, hasa baada ya Kaunti ya Nairobi kukaa kwa miezi bila naibu Gavana, wabunge wameweka wazi kuwa mswada huo ukipitishwa naibu gavana atateuliwa siku kumi nanne baada ya naibu gavana alie ofisini kufariki, kujiuzulu au kuachishwa kazi.

Aidha, Mbunge Maalum Dennitah Ghati amesema kuwa mswada huo utasaidia pakubwa kuweka wazi misingi ya kumuondoa Gavana mamalakani.

Aidha mjadala tofauti umeibuka wakati wa vikao ambapo Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani aliingia bungeni na shati iliyo na maua ya kiafrika ambayo haikuwa na kola kama ilivyo sheria na kuvaa kofia ya kiafrika.Majadla huo uliibuliwa na Mbunge wa Endebess Robert Pukose.

Duale vilevile alipinga mavazi hayo akidai kuwa kofia inayostahili kuvaliwa ni ya dini. Hatimaye Mwashetani aliondoka Bungeni.

Related Topics