Kilio cha Wamakonde chasikika

Na Beatrice Maganga

Huku uchaguzi mkuu ukikaribia, serikali imezindua mpango wa kuipa jamii ya Wamakonde vitambulisho vya kitaifa vitakavyowaruhusu kushiriki uchaguzi. Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Joseph Nkaissery amesema masaibu ya jamii hiyo inayoishi Kaunti ya Kwale yamefikia kikomo kwani itapata fursa ya kupata huduma mbalimbali za serikali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Kwale, Zainab Chidzuga ameipongeza serikali kwa kujali maslahi ya jamii zilizotengwa kwa muda.
Mshiriki wa Utawala eneo la Pwani, Nelson Marwa aidha alichukua fursa hiyo kuwarai wakazi kuendelea kushirikiana na maafisa wa usalama ili kudumisha amani, vilevile kutowatenga walioasi ugaidi na kurejea nchini kufuatia msamaha wa serikali.
Wiki iliyopita, Rais Kenyatta aliamuru kwamba Wamakonde wapewe vitambulisho vya kitaifa baada ya watu hao na wale wa jamii ya Wapemba kuandamana hadi Nairobi kuitaka serikali kuwatambua.
Jamii hizo mbili kutoka Zanzibar, Burundi na Rwanda zimekuwa humu nchini tangu mwaka 1940.