Serikali yaondoa ada za kulipia mitihani katika shule za binafsi

Na, Carren Omae

Serikali imeondoa ada za mitihani katika shule za binafsi kote nchini. Rais Uhuru Kenyatta amesema wanafunzi watakaofanya mitihani ya kitaifa katika shule za msingi na upili katika shule hizo hawatahitajika kulipia ada zozote, sawa na wale shule za umma. Wakati uo huo, Rais Kenyatta amesema serikali haitatoa mwongozo mpya kuhusu karo za shule mwaka huu.
Amesema jumla ya shilingi bilioni 29 zilizotolewa kufanikisha elimu bila malipo katika shule za kutwa za upili ziwatasaidia wanafunzi wengi kutositisha masomo yao kutokana na ukosefu wa karo. Kulingana na Rais, serikali itaendelea kutoa fedha za kutosha kufanikisha elimu nchini.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya washindi wa mashindano ya muziki ya shule katika Ikulu ya Nairobi.

 

Related Topics

uhuru kenyatta