Olo Mide Afungwa Jela

Na, Beatrice Maganga

Mwanamuziki maarufu wa Rhumba, Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha miezi kumi na minane gerezani jijini Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Mahakama ya Kinshasa vilevile imemnyima Olomide fursa ya kulipa dhamana ya pesa taslimu badala ya kuhudumu kifungo hicho kwa kumpiga teke mcheza-densi wake wa kike uwanjaji JKIA, Nairobi, Ijumaa iliyopita.
Koffi alikamatwa mapema leo nyumbani kwake jijini Kinshasa kufuatia agizo lililotolewa na Mwendesha Mashtaka wa DR Kongo. Awali mmoja wa raia wa nchi hiyo, Zakarie Bababaswe aliwasilisha kesi mahakamani akitaka mwanamuziki huyo akamatwe kwa kumdhulumu mwanadada huyo.
Olomide alirejeshwa nchini mwake kufuatia kisa cha kumdhulumu mwanabendi huyo, kisa kilichochea hisia kali ndani na nje ya nchi. Aidha alizuiwa kuwatumbuiza mashabiki wake katika ukumbi wa Bomas Nairobi, vilevile nchini Zambia.