Rais asema hakuona umuhimu wa kuhudhuria mjadala wa urais

Na, Beatrice Maganga/ John Mbuthia
Rais asema hakuona umuhimu wa kuhudhuria mjadala wa urais
Siku moja baada ya kukosa kuhudhuria mjadala wa urais, Rais Uhuru Kenyatta leo hii ameendeleza kampeni kwenye Kaunti za Murang'a na Nyeri huku akichukua fursa hiyo kufafanua sababu za kutohudhuria mjadala huo. John Mbuthia ameifuatilia ziara hiyo ya Rais na hii hpa taarifa yake.
Akihutubu katika eneo la Mukurweni ambalo hakulizuru awali wakati wa ziara yake siku chache zilizopita, Rais Kenyatta amesema alikosa kuhudhuria mjadala kwa kuwa haukona haja ya kufanya hivyo akisema maendeleo aliyowafanyia wananchi yako bayana
Uhuru ambaye amesema alimtazama Raila katika runinga wakati wa mjadala huo, amemshtumu kwa kusema hakuwa na mamlaka ya moja kwa moja ya kukabili ufisadi alipokuwa katika serikali ya mseto.
Rais Kenyatta aidha hakukosa kuvishtumu vyombo vya habari akisema havijakuwa vikimuunga mkono tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.Rais Kenyatta ameendeza ziara maeneo ya Tetu  na kuwaahidi wakazi kwamba atabuni kata mpya eneo hilo.
Katika Eneo Bunge la Othaya, Rais ameahidi kufunguliwa kwa hospitali ya Rufaa ya Othaya Februari mwaka ujao huku huduma za akina mama kujifungua bila malipo zikiendelea kuboreshwa.  
Naibu wa Rais, William Ruto ambaye ameendeleza kampeni kwenye kaunti za Vihiga na Kakamega kwa upande wake ameyakosoa madai ya Raila kuwa kuna njama ya kuwahusisha maafisa wa usalama katika kufanikisha udanganyifu wakati wa uchaguzi mkuu.

Related Topics