MSAFARA WA RAIS

Rosa Agutu

" Serikali ya Jubilee imelipa kipaumbele suala la elimu kwa wanafunzi na kutimiza ahadi ilizotoa kwa Wakenya''. Kauli hiyo imetolewa na Rais Uhuru Kenyatta alipowahutubia wakazi wa eneo la Eastlands, kabla ya kuelekea katika ukumbi wa KICC kuwasilisha stakabadhi zake za uteuzi pamoja na Naibu wake William Ruto.  Rosa Agutu na taarifa zaidi.
Awali akihutubu katika  mtaa wa Dolnholm, Rais Kenyatta amesisitiza kuwa serikali yake imejitahidi kutimiza miradi mbalimbali ya maendeleo, na kusema wanaopinga juhudi hizo hawana nia njema kwa taifa hili.

Aidha, Rais amesema wanafanya kila wawezalo ili wananchi wasiathirike na njaa kwa kuhakikisha kila mmoja anapata unga wa mahindi uliopunguzwa bei. Vilevile Rais amesisistiza kuwa taifa hili haliwezi kuendelea iwapo viongozi wataendeleza matamshi ya chuki na uchochezi ambayo yanaweza kuwagawanya wananchi kwa misingi ya kikabila.
Wakati uo huo amesema miradi iliyoanzishwa na serikali itaendelea kwani wametenga fedha za kuifanikisha. Kadhalika amesema wameweka mikakati kuhakikisha malalamishi ya kila Mkenya yanashughulikiwa.