Kinyang'anyiro kikali cha ugavana kaunti ya Kiambu

Na Beatrice Maganga


NAIROBI, KENYA, ''Hatutatangaza matokeo ya uteuzi ya ugavana Kaunti ya Kirinyaga hadi hesabu ya kura itakapokamilika''.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uchaguzi ya Chama cha Jubilee, Andrew Musangi ambaye anasisitiza kuwa watu hawafai kutoa matangazo ya uteuzi huo kabla ya kujumuishwa kwa matokeo yote ya uteuzi huo.


Hayo yanajiri huku mvutano ukishuhudiwa katika kaunti hiyo kufuatia kucheleweshwa kwa matokeo hayo. Awali aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi Ann Waiguru alidai kuwapo kwa njama ya udanganyifu.


Hayo yanajiri huku Mbunge wa Gichugu, MP. Njogu Barua, Peter Gitau wa Mwea na Stephen Ngari wa Ndia wakibwagwa wakati wa uteuzi huo, Kaunti ya Kirinyaga.

 

Related Topics