Leicester City watajikwamua?

Na Andrew Shonko
Mabingwa watetezi  wa ligi ya EPL Leicester City watakua na mlima wa kupanda leo usiku watakaposafiri kucheza dhidi ya  Sevilla katika mechi ya awamu ya 16 bora kombe la klabu bingwa barani Uropa Jumatano.

Sevilla ambao wanashikilia nafasi ya tatu katika  msimamo wa ligi ya Laliga wanashiriki mashindano haya kwa mara ya pili mfululizo. Leicester watazikosa huduma za Islam Slimani aliye na jeraha ilhali Sevillla watakua bila Gabriel Mercado, ambaye anatumikia marufuku na Nicolas Pareja  aliye na jeraha .

Katika mechi nyingine, vigogo wa Italia Juventus watasafiri  hadi Ureno kuchuana na FC Porto uwanjani Estádio do Dragão. Madifenda Andrea Barzagli na Giorgio Chiellini wanatiliwa shaka kucheza  kwa sababu ya majeraha ilhali Porto hawana jeraha lolote.
Mechi zote zitan’g’oa nanga saa 4:45