David Moyes Arejea Kazini!

Na, Stephen Mukangai

ALIYEKUWA kocha wa timu za Manchester United na Everton, David Moyes ameteuliwa kuwa meneja wa kilabu ya Sunderland. Moyes amechukua nafasi ya Sam Allardyce aliyekabidhiwa mikoba ya kuiongoza timu ya taifa ya England.

USIMAMIZI wa Sunderland umethibitisha tarifa hizo na umemtaja Moyes kuwa kocha mwenye uzoefu hasa katika ligi ya Barclays Premier.

Katika hotuba yake ya kwanza Moyes aliitaja Sunderland kuwa timu kubwa na kuwa yuko tayari kuisaidia kufanya vyema katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

KANDO na timu za Manchester United na Everton pia Moyes aliwahi kuifunza timu ya Real Sociadad ya Uhispania.