''Polisi ndio wanaoongoza kwenye visa vya dhuluma'' Yasema ripoti ya IMLU

Na Carren Omae

Maafisa wa polisi wa Kenya wametajwa kuongoza katika kuendeleza dhuluma za binadamu. Katika ripoti ya Shirika lisilo la Kiserikali, Independent Medico-Legal Unit (IMLU), asilimia 59.3 ya Wakenya wanasema mateso wanayopitia husababishwa na maafisa wa polisi.
Aidha asilimia 18.5 wanasema kuwa wanaoongoza katika visa hivyo ni Polisi wa Utawala, asilimia 13.5 wanasema ni machifu huku asilimia 8.1 wakisema ni maafisa wa usalama wa serikali za kaunti. Peter Kiama ni Mkurugenzi Mkuu wa IMLU.
Hata hivyo Msemaji wa Polisi, Charles Owino amepinga ripoti hiyo akisema utafiti mwingine wafaa kufanywa ili kuthibitisha visa hivyo. Aidha amesema idara ya polisi i tayari kuwaadhibu maafisa wa polisi wanaokiuka haki za kibinadamu.
Miongoni mwa mateso ambayo yametajwa katika ripoti hiyo ni kupigwa, kuzuiliwa katika jela zilizojaa au zenye maji, kuwazuilia wanaume na wanawake katika jela moja, kunyimwa haki ya kutafuta wakili wanapokamatwa miongoni mwa masuala mengine.