Wafanyikazi katika mashamba ya maua kuongezewa mishahara

Na Suleiman Yeri


 Mshahara wa wafanyakazi wa mashamba ya maua utaongezwa kwa asilimia ishirini na tano. Hatua hii inajiri baada ya muungano wa wakulima kutia saini makubaliano na Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi, COTU. Makubaliano hayo ni ya mwaka 2015-2016. Zaidi ya wakulima elfu sitini watanufaika na mpango huo.
Katibu Mkuu wa COTU, Franzis Atwoli amesema sekta ya maua imekuwa ikikabiliwa na changamoto chungu nzima, kama vile ada ya  juu ya umeme, kodi ya juu na gharama kubwa ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Wafanyakazi watapokea malimbikiza ya malipo ya kuanzia mwaka uliopita.