Rais Ashinikizwa Kutia Sahini Mswada wa Riba

Na Mike Nyagwoka

NAIROBI, KENYA, HUKU Wakenya wakisubiri kwa hamu kujua iwapo Rais Uhuru Kenyatta atasaini mswada wa riba kuwa sheria, viongozi mbalimbali wameendelea kumshikiza kufanya hivyo.

Gavana wa Meru ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Peter Munya amesema kuwapunguzia mzigo Wakenya mzigo wa riba ni miongoni mwa ahadi zilizotolewa na Jubilee na mswada huo utatoa nafasi nzuri ya kutimiza ahadi hiyo. Kauli sawa na hiyo imetolewa na Mbunge wa Mukurweini, Kabando wa Kabando.

Ikubukwe Rais tayari amepokea mswada huo kutoka kwa Spika wa Bunge la Taifa, Justin Muturi na sasa na siku 14 kuutia saini ama kuurejesha bungeni ili kufanyiwa marekebisho.

Mswada huo ulitayarishwa na kuwasilishwa bungeni na Mbunge wa Kiambu Mjini, Jude Njomo na unalenga kudhiditi viwango vya riba zinazotozwa ba benki.

Hata hivyo baadhi washikadau katika sekta ya benki hasa wamiliki na wakuu wa benki wamemrai Rais kutoutia saini mswada huo na badala yake kutoa fursa kwa mazungumzo kuandaliwa.

Related Topics