Policeman killed in Likoni

Ulikuwa ni usiku mrefu hapo jana kwa wakaazi wa eneo la Likoni huko Pwani pale polisi mmoja alipouwawa na watu wasiojulikana alipokuwa akishika doria,tukio lililopelekea msako kufanywa hadi hii leo huku wanaume wakilazimika kulala katika seli za polisi wakidadisiwa kuhusiana na tukio hilo lililofanyika katika eneo la majengo mapya. Visa vya maafisa wa polisi kuvamiwa vimekuwa vikifanyika mara kwa mara na hivi basi kutishia usalama katika eneo hilo