Lungalunga fire tragedy - Swahili

Watu mia moja ishirini wamethibitishwa kufariki katika kijiji cha Sinai kilichoko katika eneo la Lunga Lunga viwandani, huku takriban watu mia moja na sitini wakifikishwa katika hospitali tofauti ikiwemo hospitali kuu ya Kenyata wakiwa na majeraha ya moto. Moto huo unaaminika kusababishwa na mafuta ya petroli yaliyomwagika kutoka kituo cha kuhifadhi mafuta cha Pipeline, na kusafirishwa na mtaro wa maji ambako wenyeji wa kijiji hicho walijaribu kuyachota kabla ya mlipuko kutokea. Takriban nyumba mia tatu ziliteketea, nyingi zikiwa na watu ndani. Waziri mkuu Raila Odinga na makamu wa rais Kalonzo Musyoka walikuwa miongoni mwa viongozi waliowasili katika eneo hilo, na kuahidi kwamba serikali itawalipa fidia waathiriwa.