Ripoti Ya Ajali Ya KQ Douala

Hatimaye ripoti kuhusu kiini cha ajali ya ndege ya KQ iliyofanyika mwaka 2007, dakika chache baada ya ndege hiyo  kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Doula nchini Cameroon na kuwauwa watu 114 imetolewa. Ripoti hiyo imeelezea kinaga ubaga jinsi rubani wa ndege alivyochanganikiwa mara ilipoanza kuanguka. hata hivyo shirika la ndege la Kenya airways pamoja na serikali imesisitiza kwamba ripoti hiyo hailengi kulimbikizia mtu yeyote lawama. uchunguzi huo ulifanywa na halamashauri ya ndege nchini Cameroon.