; /* Main responsive wrapper */ .player-wrapper { width: 100%; max-width: 900px; margin: 0 auto; padding: 10px; box-sizing: border-box; } /* Ensures controls are never clipped */ #atunwa-player { width: 100%; min-height: 320px; /* KEY FIX */ } /* Mobile landscape fix */ @media (orientation: landscape) and (max-height: 500px) { #atunwa-player { min-height: 260px; } }

Zimwi la saratani ya utotoni: Uchunguzi na utambuzi wa kuchelewa unasababisha vifo

Viwango vya kuishi kwa watoto wenye saratani bado vinatofautiana sana kati ya nchi zenye kipato cha juu na zile zenye kipato cha chini, hali inayochangiwa na changamoto nyingi zinazohusiana. Moja ya sababu kuu ni ucheleweshaji au kukosa kabisa kugundua ugonjwa mapema. Uelewa mdogo wa jamii, upungufu wa vifaa na wataalamu wa uchunguzi, pamoja na watoto kufikishwa hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa, hupunguza sana nafasi ya matibabu kufanikiwa.

Tafiti za hivi karibuni zilizotolewa na The Lancet Oncology zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watoto huishi katika nchi zilizoendelea, ilhali katika nchi nyingi maskini kiwango hicho kinashuka hadi chini ya asilimia 30.

Saratani ya utotoni ni nini?

Saratani ya utotoni ni kundi la magonjwa yanayowaathiri watoto na vijana kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 19. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), saratani hizi hutofautiana na zile za watu wazima kwa kuwa mara chache husababishwa na mtindo wa maisha au mazingira. Mara nyingi hutokana na mabadiliko ya kijenetiki yanayotokea mapema wakati seli zinakua, na huenea haraka; ndiyo maana uchunguzi wa mapema na matibabu ya haraka ni muhimu.

Aina zinazopatikana zaidi

Aina za saratani zinazowapata watoto mara nyingi ni Leukemia (saratani ya damu na uboho), Uvimbe wa ubongo na mfumo wa neva na Lymphoma (saratani ya mfumo wa kinga). Nyingine ni pamoja na Neuroblastoma (huwapata zaidi watoto wadogo), Uvimbe wa Wilms (figo), Saratani za mifupa kama osteosarcoma na Retinoblastoma (jicho)

Ingawa nyingi ya saratani hizi zinaweza kutibika; na mara nyingi kupona kabisa, matokeo hutegemea sana upatikanaji wa uchunguzi wa mapema na huduma bora za afya.

Changamoto ya takwimu

Tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu kamili na zinazoaminika. Bila data sahihi, watunga sera na wataalamu wa afya hushindwa Kupima maendeleo, Kupanga rasilimali pamoja na Kubuni mikakati madhubuti ya matibabu

Mzigo wa kimataifa

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2020 na 2050, takribani watoto milioni 13.7 watagunduliwa na saratani duniani. Hata hivyo, karibu milioni 6.1 wanaweza wasigunduliwe kabisa hii ikimaanisha wengi hawatapokea matibabu kwa wakati.

Katika maeneo yenye rasilimali chache, watoto wengi hufikishwa hospitalini wakiwa katika hatua za juu za ugonjwa, hali inayopunguza uwezekano wa kupona.

Nchi zilizoendelea vs zinazoendelea

Katika nchi zilizoendelea, mafanikio ni makubwa: Marekani imeongeza kiwango cha kuishi kwa watoto wenye saratani kutoka asilimia 63 miaka ya 1970 hadi asilimia 87 kati ya 2015 – 2021, Vifo vilipungua kwa zaidi ya asilimia 50 katika miongo iliyopita

Mafanikio haya yametokana na Utafiti wa kina, Teknolojia bora za uchunguzi, Matibabu ya kisasa (chemotherapy na upasuaji) na Huduma bora za kusaidia wagonjwa

Kwa upande mwingine, katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati Viwango vya kuishi bado ni chini ya asilimia 30 kwa baadhi ya saratani, Kuna uhaba wa wataalamu, dawa muhimu, na miundombinu ya hospitali na Gharama za matibabu ni kubwa kwa familia nyingi

Hatua za kimataifa

Ili kupunguza pengo hili, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilianzisha mpango wa Global Initiative for Childhood Cancer, unaolenga Kuongeza kiwango cha kuishi hadi angalau asilimia 60 ifikapo 2030, Kuboresha uchunguzi wa mapema, Kupanua upatikanaji wa matibabu bora, Kuimarisha mifumo ya afya pamoja na Kuboresha ukusanyaji wa takwimu

Umuhimu wa uhamasishaji wa jamii

Zaidi ya sera na miundombinu, uelewa wa jamii ni muhimu sana. Katika nchi nyingi Familia hazitambui dalili za mapema na wengine hutegemea tiba za jadi kabla ya hospitali. Hali hii husababisha ucheleweshaji hatari. Kuwafundisha wahudumu wa afya kutambua dalili mapema na kuboresha mifumo ya rufaa ni hatua muhimu.

Licha ya mafanikio makubwa katika nchi zilizoendelea, watoto wengi katika nchi maskini bado wanakumbana na vikwazo vikubwa vya uchunguzi na matibabu. Mamilioni hawagunduliwi kabisa, na viwango vya kuishi bado viko chini sana ya uwezo uliopo duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, takribani watoto 400,000 hupata saratani kila mwaka duniani, huku zaidi ya vifo 78,000 vikiripotiwa mwaka 2022, wengi wao wakitoka katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

.

RELATED NEWS