;

Wakazi wa Mbukoni wanufaika na Maktaba ya Kidijitali ya WITIA

Teachers and pupils of Nkaimurunya Primary School join project partners during the launch of a digital library pilot in Gataka slum, Nairobi, Friday, Sept. 12, 2025. [File]

Wakazi wa kijiji cha Mbukoni, kaunti ya Machakos, wataanza kunufaika na mafunzo ya bure kuhusu huduma za mtandao baada ya uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa inayolenga kutoa mafunzo ya kidijitali.

Maktaba hiyo ambayo itajengwa katika shule ya Mbukoni Comprehensive School inalenga kutoa mafunzo kwa wanafunzi wakati wakiwa shuleni, huku pia wakazi wakipata fursa ya kutumia rasilimali hizo wakati wa likizo.

Ujenzi wa maktaba hii umefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Women in Technology and Innovation Africa (WITIA).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mwanzilishi wa shirika hilo, Eunice Pohlmannalisema lengo ni kusaidia wanafunzi na wakazi kuelewa na kutumia mitandao kwa ufanisi. Aliongeza kwamba kuna fursa nyingi za ajira kwenye sekta za kidijitali, na hivyo ni muhimu kuwafundisha vijana kutumia mitandao wakiwa na umri mdogo ili kujijenga kiuchumi.

“Kwa wakazi, pia ni muhimu kuwa na uelewa wa mitandao, hasa kwa kuwa huduma nyingi za serikali sasa zinapatikana mtandaoni kupitia mfumo wa e-Citizen,” alisema Pohlmann.

Meneja wa mradi wa ujenzi wa maktaba za WITIA, Wesa Sitati, alisema mradi huu ni sehemu ya mpango wa kujenga maktaba sawia katika shule mbalimbali nchini, na mradi wa Mbukoni ni wa pili kufuatia mafanikio ya mradi wa awali katika kaunti ya Turkana. Alisema wanahamasisha wanafunzi na wanakijiji kutumia maktaba hizo ipasavyo ili waweze kufaidika kikamilifu.

Maktaba hizo, zenye gharama ya ujenzi ya kati ya shilingi milioni 5 – 7, zimepewa jina la WITIA Smart Library ProjectAidha, WITIA wameahidi kufadhili masomo ya wanafunzi bora kutoka kila shule itakayohusishwa na mradi huo hadi kufikia elimu ya chuo kikuu.

.

RELATED NEWS