Wazee Wasuba katika mojawapo ya ngoma zao asilia. Jamii ya Suba inafurahia kuwasilishwa bungeni na mmoja wao Mbunge John Mbadi.
Kuna makabila mengine ya zamani ambayo yamebakia na watu wachache tu wanaofahamu asili mila na desturi za wavyele wao. Hii ni kutokana na uhamaji na kumezwa na makabila mengine. Wasuba ama Abasuba ni moja ya makabila ya watu wa Kenya ambao wanaongea lugha ya Kisuba lakini wengi wao huongea Kijaluo. Jina Suba huwakilisha makundi matatu tofauti ya watu wanaoishi Kusini Magharibi mwa Kenya katika eneo la Nyanza Kusini na mamkundi hayo ni Suba (Abasuba) Irenyi (abirienyi ) na Kunta (Abakunta). Kundi la Suba liliingia Kenya kutoka eneo la Mara Tanzania. Ingawa Wasuba huchukuliwa kama kabila, wao ni kabila dogo tu lililokuwa chini ya kabila kubwa la Wagirango lililojumuisha makabila mengine madogo kama vile Wategi na Wagire.