Kivumbi kinatarajiwa bungeni Alhamisi alasiri wakati Mswada wa Kifedha wa Mwaka 2023, utakapowasilishwa kusomwa kwa mara ya pili. Kisha wabunge watapata fursa ya kuujadili ambapo ubabe baina ya wabunge wa Kenya Kwanza na Azimio unatarajiwa kushuhudiwa.
Mswada huo wa Kifedha utawasilishwa na Kiongozi wa Wengi wa Bunge la Kitaifa Kimani Ichungwa ambaye jukumu lake kuu ni kuzisukuma ajenda za serikali bungeni.