Premium

Papa Benedict XVI amezikwa

Aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Benedict wa kumi na sita amezikwa.

Papa Benedict amezikwa baada ya misa iliyoongozwa na Kiongozi wa Sasa wa Kanisa hilo, Papa Francis na imefanyika katika Kanisa la St. Peters Squire, Vatican.

Maelfu ya watu waliohudhuria mazishi hayo ni wakiwamo viongozi mashuhuri kutoka familia za kifalme kote Uropa kama vile Uingereza, Uhuspania, Ujerumani na Ureno.

Aidha, wawakilishi kutoka madhehebu mbalimbali kama vile, Orthodox, Lutheran, Muunganao wa Makanisa ya Kievanjelisti Duniani, Wayahudi na Waslamu wamehudhuria.

Baada ya ibada ya buriani, Jeneza lenye mwili wa Papa Benedict wa kumi na sita limewekwa kwenye sanduku la chuma na kupelekwa katika makaburi yaliyoko chini ya Kanisa Kuu St. Peters.

Hafla hiyo ya maziko imefanyika faraghani kwa kuwa alijuzulu kabla ya kukamilisha hatamu ya uongozi, Papa Benedict wa kumi na sita hajazikwa na Fimbo la Kiaskofu, badala yake ndani ya sanduku kumewekwa sarafu za wakati wa uongozi wake, waraka unaosimulia kwa ufupi uongozi wake pamoja na Pallio Takatifu yaani kitambaa kinachotengenezwa kutumia manyoya ya kondoo wachanga kinachovaliwa na papa shingoni.

Mwili wa Papa Benedict wa kumi na sita umezikwa katika kaburi la kwanza la Papa John Paul wa Pili lililoko sehemu ya chini ya Kanisa la St. Peters. Mwili wa Papa John Paul uliondolewa kwenye kaburi hilo na kuhamishiwa kwenye kaburi jingine lililoko ndani baada ya kutawazwa kuwa Mtakatibu mwaka 2014 katika utaratibu ulioanza mwaka 2011.

Kuna zaidi ya makaburi 90 ndani ya Kanisa la St. Peters ambako mili ya Papa waliotangulia imezikwa.

Papa Benedict wa kumi na sita aliyekuwa na umri wa miaka 95 alifariki dunia wiki jana. Alichaguliwa kuwa Papa mwaka 2005 kufuatia kifo cha Papa John Paul wa Pili lakini akajiuzulu mwaka 2013 kutokana na sababu za kiafya. Alikuwa Papa wa Kwanza katika Kipindi cha miaka mia sita kufanya hivyo.