Rais William Ruto ametimiza ahadi yake ya kuwaapisha majaji sita walioachwa nje wakati wengine arobaini walipoapishwa na Rais Mstaafu, Uhuru Kenyatta. Akizungumza wakati wa halfa hiyo katika Ikulu ya Nairobi ambayo pia imehudhuria na aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga wakati uteuzi wa majaji hao ulipokataliwa na Uhuru, Rais Ruto amesisitiza umuhimu wa kuiheshimu Idara ya Mahakama na idara nyingine huru na kuzipa nafasi ya kutekeleza majukumu yao bila mwingilio.
Ruto ametoa changamoto kwa Idara ya Mahakama kuzishughulikia kwa wakati hasa kesi za ufisadi ambazo anasema zimekuwa zikichukua muda mrefu mahakamani.