×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Polisi Nairobi watibua sherehe ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kiongozi wa upinzani Bobi Wine

12th February, 2022

Polisi jijini Nairobi wametibua sherehe iliyoelezewa kuwa ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi Al Maarufu Bobi Wine. Polisi kutoka kituo cha Kilimani walivamia mkahawa mmoja katika eneo la Upper Hill Nairobi, wakisema kuwa waliopanga karamu yenyewe hawakuzingatia sheria kwa kukosa kutafuta kibali kutoka kwa polisi. Karamu hiyo ilihudhuriwa na kakake Wine, Fred Nyanzi miongoni mwa jamaa zake. Sherehe hiyo ilitazamiwa kuhudhuriwa na wabunge kutoka upinzani ila hawakufika. Wine alikuwa mshindani wa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa mwaka jana na kuibuka wa pili. Alipinga matokeo ya uchaguzi huo kwa kudai wizi wa kura.

.
RELATED VIDEOS