.
27th January, 2022
Naibu Rais William Ruto, amekita kambi katika kaunti ya Kiambu, akilenga kuhifadhi uungwaji mkono katika eneo la Mlima Kenya.
Ruto ambaye hakuandamana na wandani wake wapya kisiasa, kinara wa ANC Musalia Mudavadi na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetang'ula, alisema muungano wao mpya utashinda kiti cha Urais katika raundi ya kwanza, katika uchaguzi mkuu wa agosti mwaka huu.