7th July, 2021
Familia ya koplo Caroline Kangogo afisa wa polisi mtoro anayeeaminika kuteekeleza mauaji ya watu wawili akiwemo afisa wa polisi mwenye cheo cha konstebo imemtaka ajisalimishe kwa maafisa wa polisi na kuomba msamaha familia zilizofiwa kwa niaba ya mwana wao. Wakazi wa kijiji cha nyawa kaunti ya Elgeyo Marakwet alikozaliwa Caroline leo walijumuika katika maombi wakiwa na tumaini kuwa afisa huyo wa polisi atapata utulivu na kujisalimisha. Na kama anavyoripoti mwanahabari elvis kosgei maafisa wa polisi wamezingira boma la afisa huyo.