27th January, 2021
Huku wakenya wakiendelea kukabiliana na janga la korona mashirika yasiyokuwa ya serikali yamesema ipo haja ya kuwalea na kuwatunza watoto wanaorandaranda mijini,kutokana na makali ya virusi hivyo.akizungumza katika eneo la langas huko Eldoret kaunti ya Uasin Gishu, kasisi gichuhi njoroge amesema ni jukumu la kila idara husika ya kutafuta njia mbadala ya kuzikidhi familia hizi. eneo la mji wa eldoret lina watoto wengi wa kurandaranda ambao kuna wakati walifurushwa.