.
8th November, 2020
Katibu wa kina mama wanachama wa KANU tawi la Nairobi Betty Adera amesema chama hicho kimeimarisha mikakati ya kukifufua na sasa kiko imara na kitakuwa na wagombeaji viti katika maeneo yote kaunti ya nairobi kwenye uchaguzi mkuu ujao. Adera alikuwa akizungumuza eneo la Embakasi hapa nairobi wakati wa uzinduzi wa afisi mpya ya chama hicho katika maeneo hayo.