.
8th November, 2020
Mgombea wa Democrat Joe Biden ambaye aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa urais nchini marekani ameahidi kuleta umoja nchini humo baada ya uchaguzi ulioshuhudia mgawanyiko mkubwa. Hayo yanajiri huku Rais Donald Trump aliyewania kwa tiketi ya Republican akikataa kukubali matokeo hayo. Ushindi wake ukikamilisha siku 4 za kusubiri matokeo ya uchaguzi huo na kuanzisha sherehe miongoni mwa wafuasi wake Biden na Kamala Harris kufurahia ushindi wao. Hebu tupate kwa kifupi hotuba walizotoa Biden na Kamala baada ya kuibuka washindi.