20th June, 2020
Janga la korona limeathiri sekta mbalimbali za uchumi, wafanyabiashara wadogo wakiwa miongoni mwa waliopata pigo kubwa. Wafanyabiashara wa masoko ya Gikomba na Mtindwa jijini nairobi wanakadiria hasara kufuatia marufuku dhidi ya bidhaa za mitumba. Brian otieno anaripoti kuhusu hayo katika siku ambayo idadi ya walioambukizwa virusi vya korona ikiendelea kupanda na idadi ya vifo ikifika watu 121 baada ya watu wawili zaidi kufariki dunia.