.
3rd June, 2020
Gavana wa nairobi mike sonko ametia saini bajeti ya ziada ya shilingi bilioni tatu nukta tano itakayoelekezwa kwa huduma ya jiji la nairobi almaarufu nairobi metropolitan services. Takriban bilioni mbili zimetengewa matumizi ya kila siku huku bilioni moja nukta mbili ikitengewa shughuli za maendeleo jijini zinazoendelea kutekelezwa na huduma hiyo pamoja na matumizi ya kila siku. Akizungumza katika ofisi ya kibinafsi ya gavana sonko eneo la upper hill jijini nairobi, msemaji wake ben mulwa amesema kuwa maendeleoyanayoendelea kushudiwa yalianzishwa na serikali ya gavana sonko.