x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Aisha Jumwa atimuliwa kutoka kwenye tume inayosimamia masuala ya bunge

28, May 2020

Wabunge wa mrengo wa NASA wamefanya kikao cha bunge ambapo waliamua kwa kauli moja kuwatimua wabunge tisa kutoka kamati za bunge.  Mbunge wa Kiminini Chrisantus Wamalwa ametimuliwa kama naibu kiranja wa wachache katika bunge la taifa na mahala pake kuchukuliwa na Mbunge wa Tongaren David Eseli Simiyu.     Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ametimuliwa kama kamishna kwenye tume inayosimamia masuala ya bunge na ikapendekezwa nafasi hiyo ichukuliwe na mbunge wa Likoni, Mishi Mboko.  Kiongozi wa wachache katika bunge la taifa, John Mbadi amesema utaratibu wa kumtimua Aisha Jumwa kirasmi umeanza.

Feedback