Chemichemi za ziwa: Watu wahama makazi yao baada ya ziwa Nakuru kuchipuka kutoka chini
20, May 2020
Mwezi mmoja baada ya wakazi wa mwariki katika kaunti ya nakuru kuelezea hofu kuhusu maji ya ziwa nakuru kuingia makazi yao kutokea ardhini, sasa wameanza kubomoa makazi yao na kupangisha vyumba mjini nakuru. Hii ni kutokana na maboma yao kutota maji huku wanasayansi wakionya kuwa huenda hali hiyo iwe mbaya zaidi kwani ziwa nakuru linarejelea nafasi yake.