.
23rd February, 2020
Watu Kadhaa Wanauguza Majeraha Baada Ya Kushambuliwa Na Wezi Katika Mtaa Wa Kofi Anan Kapsoya Mjini Eldoret Jana Usiku. Wezi Hao Walivunja Milango Na Kuibia Wakazi Mwendo Wa Saa Saba Usiku Huku Mkazi Mmoja Akiachwa Na Majeraha Mabaya Ya Upanga.Kulingana Na Wakazi Wezi Hao Walikua Na Mda Wa Kutosha Kwani Walivamia Nyumba Hadi Nyumba Na Hata Nduru Za Wakazi Hazikuwatisha. Licha Ya Jitihada Zao Kuwafikia Maafisa Wa Polisi, Hakuna Msaada Wowote Uliowafikia Hali Inayowaacha Na Hofu Zaidi. Hadi Sasa Maafisa Wa Polisi Kutoka Kituo Cha Kapsoya, Inaarifiwa Kuwa Bado Hawajafika Kuanzisha Uchunguzi Wao.