.
17th February, 2020
Kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Daktari Ekuru Aukot ametangaza mwanzo wa awamu ya pili ya kukusanya sahihi ili kurekebisha katiba chini ya kauli mbiu ’punguza mizigo’. Aukot ameyagawanya mageuzi hayo katika viwango kumi ikiwemo kuupa nguvu ugatuzi, kuiondoa seneti, kupunguza idadi ya wabunge pamoja na kuipa nguvu zaidi bunge kati ya mapendekezo mengine. Wakati uo huo Aukot amezindua njia ya kidijitali ya wakenya kutia sahihi kuunga mkono mabadiliko hayo ya katiba. ?