27th January, 2020
Visa vya mikosi inayohusishwa na hali ya hewa vimekithiri katika sehemu nyingi duniani. Katika bara la afrika, ukame na mafuriko ni majanga yaliyoongezeka yakisababisha maafa na uharibifu wa maendeleo. Jijini Mombasa takriban wanahabari kutoka nchi 20 za afrika wanajumuika hii leo kwa kongamano la kujadili mawasiliano wakati wa hatari. Warsha hiyo ya siku nne imeandaliwa na muungano wa wanahabari wanaojihusisha na masuala ya hatari barani Afrika kwa ufadhili wa umoja wa mataifa kitengo cha Kukabiliana na majanga.