26th January, 2020
Mgogoro wa uongozi umezuka katika kanisa la Kimethodisti eneo la Kongowea Mombasa na kuwalazimisha waumini kufanya ibada ya jumapili nje ya kanisa hilo. Waumini walilazimika kukaa nje baada ya polisi kulizingira kanisa hilo na kuzuia mtu yeyote asiingie.