22nd January, 2020
Wataalam pamoja na maafisa wa serikali wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na idadi ndugo ya wanawake wanaojitokeza kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa uzazi. Wataalamu hao wamesema hayo baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umma kuhisiana na aina hiyo ya saratani katika kaunti ya Makueni. Kamishna wa kaunti ya Makueni Mohammed Maalim amewataka machifu kusaidia katika kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kuhusiana na ugonjwa huo