Magoha akariri msimamo wa serikali ya kuwataka walimu wakuu kuruhusu wasio na karo kujiunga na shule

KTN News Jan 22,2020


View More on KTN Leo

Waziri wa elimu profesa George Magoha amekariri msimamo wa serikali wa kuwataka walimu wakuu wa shule za upili kutowazuia  wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza kwa sababu ya ukosefu wa karo. Magoha ameyasema hayo katika kampeni inayoendelea ya kuahakikisha kuwa wanafunzi wote wanajiunga na kidato cha kwanza ambapo alimtembelea mwanafunzi mmoja katika eneo la njiru hapa jijini Nairobi na kisha kumsindikiza kujiunga na shule ya upili katika kaunti ya Machakos.