Visiwa viwili kaunti ya Kwale vitanufaika na mradi wa Kawi ya umeme

KTN News Jan 13,2020


View More on KTN Leo

Visiwa viwili katika kaunti ya kwale vya mkwiro na wasini vilivyoo lungalunga,  vinatarajiwa kunufaika na mradi wa umeme utakaofadhiliwa na benki ya duina na kaunti ya kwale  Kulingana na meneja msimamizi wa shirika moja lisilo la kiserikali mradi huo wa milioni 100 utazalisha kawi kupitia miale ya jua, na kuleta umeme katika visiwa hivyo. Wakizungumza baada ya mkutano wao, gavana wa kwale Salim Mvurya amesema mradi huo utawafaidi wenyeji ambao hutegemea sana uvuvi kuimarisha biashara ya samaki. Mradi huo utakaochukua miezi 12 ni mmoja wa miradi ya benki ya dunia katika kaunti yak wale.