13th January, 2020
Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi ili kuwatawanya wanafunzi wa chuo kikuu cha Egerton waliokuwa wakizua rabsha nje ya chuo hicho. Wanafunzi hao walianzisha fujo kulalamikia hatua ya usimamizi wa chuo kuwazuia kuingia shuleni humo kabla ya kulipa pesa za gharama ya uharibifu waliosababisha kwenye mgomo wao wa Disemba mwaka jana.