Kiwanda cha Webuye yakosa kufanya kazi kwa ukosefu wa umeme

KTN News Jan 11,2020


View More on KTN Leo

Bodi ya wasimamizi wa chuo cha ufundi cha webuye west technical vocational college, katika kaunti ya bungoma, inaitaka serikali ya taifa kuingilia kati ili kuwezesha kiwanda kilichojengwa kwa ufadhili kutoka serikali ya uchina kianze kufanya kazi. Kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali yakiwamo maziwa na nyama, kilijengwa kwa gharama isiyopungua shilingi milioni mia moja, ila hakijakuwa kikifanya kazi kufuatia ukosefu wa umeme.