Mwili wa mwanahabari Anjlee Gadhvi yateketezwa katika tanuri ya Kihindi Kariakor

KTN News Jan 11,2020


View More on KTN Leo

Mwili wa mwanahabari wa runinga ya k 24 Anjlee Gadhvi umeteketezwa hii leo katika tanuri la kihindi iliyoko mtaa wa Kariokor jijini Nairobi.  Ibaada ya wafu ilifanyika katika ukumbi wa Lohana ulioko Forest Road, Mstakabala na Nairobi Gymkhana.
Marehemu Anjlee aliwahi kufanya kazi na shirika la KTN News kabla kujiunga na k 24.  Aliaga dunia siku ya ijumaa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi.  Jamaa na marafiki walijumuika kwenye ibaada ya wafu kutoa heshima zao za mwisho.  Marehemu Anjlee alikuwa akiuguza saratani ya mapavu na maini.  Aligunduliwa na saratani mwaka wa 2013 kufuatia uchunguzi kwa maabara.  Anjlee alifanyiwa matibabu humu nchini na nje ya nchi.  Mwaka 2018 alisafiri nchini india kupokea matibabu spesheli kwa jina ‘cyberknife procedure’ kwa minajili ya kupambana na kuangamiza saratani mwilini. Marehemu anjlee amemuacha mume na watoto wawili.