Sonko kumteua Ann Kananu kama Naibu wake juzi kumezua Utata miongoni wa Viongozi

KTN News Jan 08,2020


View More on KTN Leo

Baraza La Magavana Hii Leo Limesema Limeunga Mkono Hatua Ya Gavana Wa Nairobi Mike Sonko Kumteua Naibu Wake Huku Wakisema Hatua Hiyo Ni Haki Ya Kisheria. Aidha, Gavana Sonko Kupitia Wakili Wake Amemuandikia Barua Mkurugenzi Mkuu Wa Mashtaka Ya Umma Noordin Haji Akisema Kuwa Hatua Yake Ya Kumteua Naibu Wake Hajakiuka Masharti Ya Dhamana Yake  Alivyokuwa Amedokeza Haji. Wakati Huo Huo Misimamo Kinzani Imezuka Katika Bunge La Kaunti Ya Nairobi Huku Baadhi Ya Wawakilishi Wadi Wakiunga Mkono Hatua Ya Sonko Na Wengine Wakipinga Vikali. Isitoshe Baadhi Wamemshtumu Spika Wa Kaunti Ya Nairobi Beatrice Elachi Kwa Maadai Ya Kutaka Kunyakua Majukumu Ya Gavana.