Mwalimu adaiwa kushiriki mahaba na mwanafunzi wake kisha kuweka picha zao za uchi mitandaoni

KTN News Jan 07,2020


View More on KTN Leo

Familia moja huko Bungoma inaitaka tume ya kuwajiri walimu, TSC, kumchukulia hatua mwalimu mmoja wa shule ya msingi, anayedaiwa kufanya mapenzi na binti yao kisha kumpiga picha akiwa uchi na kuzitundika picha hizo mitandaoni. Mwalimu huyo kutoka shule ya msingi ya Namutokholo, huko Sirisia          kaunti ya Bungoma, anatuhumiwa kumpiga picha mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu akiwa uchi, na kisha kuzitundika picha za mwanafunzi huyo kwenye mtandao. Babake msichana huyo aliaga dunia hivi majuzi na inadaiwa kwamba mwalimu huyo aliahidi kwamba angemsaidia msichana huyo.