4th January, 2020
Wakazi Wa Kijiji Cha Nyabworoba Kaunti Ya Kisii Wameeleza Hofu Ya Watoto Wao Kukosa Masomo Shule Zinapofunguliwa Juma Lijalo, Baada Ya Kuhama Makazi Yao Kutokana Na Maporomoko Ya Ardhi Eneo Hilo. Wakazi Hao Wapatao Mia Moja Na Hamsini Wa Wadi Za Sensi Na Chitago Borabu Walihamishiwa Shule Ya Msingi Na Nyabworoba Sekondari, Kwenye Shughuli Iliyosimamiwa Na Kamishna Wa Kaunti Ya Kisii Stephen Kihara.