31st December, 2019
Mkuu wa upelelezi George Kinoti amevunjilia mbali kitengo cha Flying Squad kilichoongozwa na afisa Musa Yego. Maafisa waliokuwa chini ya kitengo hicho wamepelekwa kwenye vitengo vingine na kitengo chenyewe kupewa jina jipya la The Sting Squad.