Wakaazi wa Samburu wanaishi kwa hofu la kutishiwa na simba

KTN News Dec 28,2019


View More on KTN Leo

<style type="text/css">p.p1 {margin: 0.0px 0.0px 0.0px 0.0px; line-height: 20.1px; font: 15.0px 'Microsoft Sans Serif'} span.s1 {font: 10.0px Arial} span.Apple-tab-span {white-space:pre} </style>

    Wakaazi wa kijiji cha Nkutoto arus kaunti ndogo ya Samburu Kaskazini wanaishi kwa hofu baada ya kundi la simba wanane kuhepa hifadhi za wanyama pori na kuvamia kijiji hicho huku wakishambulia na kuwaua mifugo wao. Simba hao wanadaiwa kuwaua zaidi ya ngombe ishirini na Mbuzi ambao idadi yao haijabainishwa kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita. Sasa wenyeji hao wanalaumu shirika la wanyamapori, KWS, kwa kupuuza malalamishi yao na sasa wanaitaka serikali kuingilia kati wakionya kuchukua sheria mikononi mwao iwapo hatua haitachukuliwa.