18th December, 2019
Kesi ya jinai inayomkabili gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko dhidi ya polisi imekosa kung’oa nanga katika mahakama ya Voi kwa kuwa Sonko hakuwepo kuitikia mashtaka matatu ya kujeruhi afisa wa polisi, kudinda kukamatwa na kutatiza amani. Mahakama ilielezwa kuwa Sonko angali anauguza majeraha na kuwa anahitaji muda zaidi kufika mbele ya hakimu mkuu Mkazi F. Nyakundi.