.
17th December, 2019
<style type="text/css">p.p1 {margin: 0.0px 0.0px 0.0px 0.0px; line-height: 20.1px; font: 15.0px 'Microsoft Sans Serif'} span.Apple-tab-span {white-space:pre} </style>
Zaidi ya familia elfu mbili katika kaunti ya Nakuru zimeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika sehemu tofauti nchini . Maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Molo, Kuresoi Kaskazini, Subukia na Ndabibi,Naivasha na tayari vifo vya watu 15 vimeripotiwa. Zaidi ya familia tisini zilipoteza makazi katika kijiji cha Ndabibi huko  Naivasha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la Maela na Narok.