MARADHI YA AJABU: Jinsi ugonjwa wa mapumbu/ngirimaji unavyowahangaisha wanaume Kilifi

KTN News Dec 16,2019


View More on KTN Leo

Ugonjwa wa mapumbu au ngiri maji unaendelea kuwa tishio la kiafya kwa wanaume wengi eneo la pwani na zaidi kaunti ya Kilifi. Katika kaunti hii baadhi ya waume wameachwa na wake zao huku ndoa zikivunjika sababu kuu kutotosheleza haki zakindoa. Ni ugonjwa adimu ila wa kutisha kwani unafurisha na kuvimbisha sehemu za siri na kumuacha muathiriwa kuonekana kama amebeba mzigo katikati ya miguuni pake. Mwanahabari wetu wa Pwani Tobias Chanji alitangamana na baadhi ya wagonjwa hawa wakati wa kambi ya matibabu katika kaunti ya Kilifi na kuandaa taarifa ifwatayo.