.
11th December, 2019
  Mvulana mmoja huko elgeyo marakwet amepigwa na butwaa baada ya kupokea barua ya mwaliko wa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya wasichana. Cherono Timothy Kiptoo ameelezea mshangao wake kwani haelewi ni vipi yeye akiwa mvulana alipata mwaliko wa kujiunga na shule ya wasichana ya sing'ore. Wazazi wa mvulana huyo sasa wanamtaka waziri wa elimu, Prof George Magoha, amnusuru mwana wao.